Posts

AKIMBIWA NA NDUGU ZAKE

Image
@fmfacts Baada ya Eknath Gawali (54) Mwanaume Raia wa Aurangabad, India Kufanyiwa Upasuaji Hospitalini Mei 2018, Ilimbidi Binti Yake wa Miaka 9 Ashirikirie Dripu la Maji kwa Masaa Mawili Bila Kushusha Kutokana na Hospital Hiyo Kukosa Vifaa, Watoto Wake Wengine Walimkimbia Kumuuguza.

KIFO NDIO KIWATENGENISHE

Image
Tangu Mwaka 1954, Kwa Mujibu wa Sheria za Nchini Ufilipino, Njia Pekee ya Kuachana na Mumeo au Mkeo wa Ndoa ni Kifo tuu, Hakuna Kupeana Talaka. Ufilipino Ndio Nchi Pekee Duniani Ambayo Sheria Hairuhusu Talaka, Kuachana Kwenu ni Mpaka Kifo Pekee Japo Dini Zinapinga Hili.

DEAL WANALOPIGA HAWA CELEBRITY

Image
Image
From @ fmfacts Kama kuna simulizi ya kukukumbukwa inayowatoa machozi raia wengi wa Colombia hasa wa miji ya Caldas na Tolima basi ni hii ya mtoto wa kike wa umri wa miaka 13 Omayra Sanchez iliyomtokea mwaka 1985.  Omayra alikuwa ni mtoto aliyezaliwa August 28, 1972 huko Colombia na alifariki November 16, 1985 kwa mateso makali akiwa na umri wa miaka 13 huko Armero Columbia baada ya kukwama kwa siku 3 kwenye shimo lenye lava  kutokana na mlipuko wa Volcano uliotokea. Janga hilo la volcano lililopewa jina la Nevado Del Ruiz lilitokea November 13, 1985 na kusababisha vifo vya zaidi ya Watu 25,000 Huku binti huyu wa miaka 13 pekee akikwama kwenye shimo ambapo volcano hiyo ilipita, unaweza kuvuta picha ya maumivu makali aliyoyapitia binti huyu. Wakati mlipuko unaanza binti Omayra aliusikia, na alipokua anajitahidi kukimbia ili aepukane nao ndipo kwa bahati mbaya alijikuta ameingia ndani ya shimo lililopo karibu na nyumba yao, shimo ambalo lilikua na maji mengi pamoja na volcano dani yake, y...

AJIUA KISA MGAHAWA WAKE KUSHUKA UBORA

Image
From @ fmfacts Baada ya Mgahawa Wake wa Gusteau Kushushwa Hadhi Kutoka Hadhi ya Nyota 5 Hadi Nyota 3 Mwaka 2003 kwa Kufanyiwa Figisu na Mmoja wa Wapishi Wake Aliyewahi Kufanya Kazi Hapo, Mpishi Maarufu wa Ufaransa Bernard Loiso Aliyekuwa Anaumiliki Mgahawa Huo Akajiuwa. Bernard alikuwa ni mpishi mashuhuri nchini ufaransa na mwenye talanta kubwa ya upishi ambaye mwanzoni mwa miaka ya 2000 alianzisha mgahawa wa Gusteau, ambao haraka ukapewa hadhi ya nyota tano. Kauli mbiu yake ya kibinafsi ilikuwa ni kwamba mtu yeyote anaweza kupika, alikuwa mpishi mdogo katika historia katika nchi hiyo kupata mgahawa wenye nyota 5, na alikuwa miongoni mwa wapishi bora zaidi ulimwenguni. Mgahawa huo ulipoteza moja kati ya nyota zake tano na kushushwa hadi nyota tatu baada ya mwaka 2003 mkosoaji mkuu wa chakula wa Ufaransa Anton Ego kuandika mambo machafu juu ya mgahawa huo akisema kuwa anafahamu siri zote kwakuwa yeye pia aliwahi kufanya kazi ya upishi hapo. Bernard alivunjika moyo kutokana na mgahawa w...

MFAHAMU MBAKAJI WA NGURUWE

Image
From @ fmfacts Baada ya Cody Slaughter Raia wa Yuma Arizona US Kukamatwa kwa Kumbaka Mtoto wa Miaka Miwili, Kumbaka Nguruwe, Mbwa na Farasi, Akakimbia Polisi Wakati Kesi Ikiendeelea. Mwaka 2012 Akapeleka Vyeti Vyake Kuomba Kazi Serikalini, Akakamatwa. Ilikuwa ni July 12, 2012 ambapo mji wa Somerton, Arizona US ulikuwa unatafuta vijana wa kuwasomesha na kuwaajiri kwa kazi ya doria, kulinda mipaka ya nchi hiyo, mmoja wa vijana waliopeleka maombi ya kazi hiyo alikua ni Cody Slaughter. Kijana huyo wa umri wa miaka 22 ilibidi akamatwe na polisi baada ya kupitia documents zake na kujua kuwa alikuwa ni mhalifu aliyetoroka Polisi ambapo hata alipokamatwa na kuhojiwa alikiri kuwa aliwahi kumdharirisha kingono mtoto wa umri wa miaka 2 miaka 8 iliyopita akiwa na miaka 14. Mbali na hilo pia Cody alikiri kuwa alikuwa na maingiliano ya ngono na mbwa, farasi na nguruwe, na alikuwa na historia ya utumiaji wa dawa za kulevya na baadaye mchinjaji. Licha ya kubainika na makosa hayo aliyoyafanya kati ya m...

Saddam Hussein|mtu akatwe mikono tu

Image
Akiwa Rais wa Iraq, Mwaka 1994 Saddam Hussein Alisign Adhabu ya Kupigwa Chapa Isiyofutika Usoni na Kukatwa Mikono, Miguu au Masikio Kama Utabainika Umeiba au Umehusika na Rushwa. Afisa Mmoja Alipigwa Chapa, Akaenda Kuifuta Hospitali, Madaktari Wote nao Wakakamatwa na Kukatwa Mikono. Mwaka 1997 Hussein Alitangaza Kuwa Ameandika Kitabu cha Qur'an kwa Kutumia Lita 27 za Damu Yake Aliyotumia Miaka 2 Kuitoa. Kuanzia Juni 4, 1994 serikali ya Iraq chini ya Saddam Hussein ilitoa amri tisa ambazo zikikiukwa tuu adhabu yake ilikuwa ni kali kama vile kukatwa viungo vya mwili, kupigwa chapa au adhabu ya kifo, baadhi ya  makosa yaliyopelekea adhabu hizo ni kama vile wizi, ufisadi au rushwa. Amri hizi mpya ziliathiri sana haki za binadamu lakini serikali ya Iraq ilipuuza ukosoaji mkubwa wa kimataifa wa ukatili huu kwa kusema kwamba amri hizo zilitungwa ili kupambana na uhalifu nchini humo ambapo unaleta vikwazo vya kiuchumi. Miaka hiyo ya 1990 afisa mmoja wa nchini humo alituhumiwa kwa rushwa na...