Posts

Showing posts from September, 2020

DEAL WANALOPIGA HAWA CELEBRITY

Image
Image
From @ fmfacts Kama kuna simulizi ya kukukumbukwa inayowatoa machozi raia wengi wa Colombia hasa wa miji ya Caldas na Tolima basi ni hii ya mtoto wa kike wa umri wa miaka 13 Omayra Sanchez iliyomtokea mwaka 1985.  Omayra alikuwa ni mtoto aliyezaliwa August 28, 1972 huko Colombia na alifariki November 16, 1985 kwa mateso makali akiwa na umri wa miaka 13 huko Armero Columbia baada ya kukwama kwa siku 3 kwenye shimo lenye lava  kutokana na mlipuko wa Volcano uliotokea. Janga hilo la volcano lililopewa jina la Nevado Del Ruiz lilitokea November 13, 1985 na kusababisha vifo vya zaidi ya Watu 25,000 Huku binti huyu wa miaka 13 pekee akikwama kwenye shimo ambapo volcano hiyo ilipita, unaweza kuvuta picha ya maumivu makali aliyoyapitia binti huyu. Wakati mlipuko unaanza binti Omayra aliusikia, na alipokua anajitahidi kukimbia ili aepukane nao ndipo kwa bahati mbaya alijikuta ameingia ndani ya shimo lililopo karibu na nyumba yao, shimo ambalo lilikua na maji mengi pamoja na volcano dani yake, y...

AJIUA KISA MGAHAWA WAKE KUSHUKA UBORA

Image
From @ fmfacts Baada ya Mgahawa Wake wa Gusteau Kushushwa Hadhi Kutoka Hadhi ya Nyota 5 Hadi Nyota 3 Mwaka 2003 kwa Kufanyiwa Figisu na Mmoja wa Wapishi Wake Aliyewahi Kufanya Kazi Hapo, Mpishi Maarufu wa Ufaransa Bernard Loiso Aliyekuwa Anaumiliki Mgahawa Huo Akajiuwa. Bernard alikuwa ni mpishi mashuhuri nchini ufaransa na mwenye talanta kubwa ya upishi ambaye mwanzoni mwa miaka ya 2000 alianzisha mgahawa wa Gusteau, ambao haraka ukapewa hadhi ya nyota tano. Kauli mbiu yake ya kibinafsi ilikuwa ni kwamba mtu yeyote anaweza kupika, alikuwa mpishi mdogo katika historia katika nchi hiyo kupata mgahawa wenye nyota 5, na alikuwa miongoni mwa wapishi bora zaidi ulimwenguni. Mgahawa huo ulipoteza moja kati ya nyota zake tano na kushushwa hadi nyota tatu baada ya mwaka 2003 mkosoaji mkuu wa chakula wa Ufaransa Anton Ego kuandika mambo machafu juu ya mgahawa huo akisema kuwa anafahamu siri zote kwakuwa yeye pia aliwahi kufanya kazi ya upishi hapo. Bernard alivunjika moyo kutokana na mgahawa w...

MFAHAMU MBAKAJI WA NGURUWE

Image
From @ fmfacts Baada ya Cody Slaughter Raia wa Yuma Arizona US Kukamatwa kwa Kumbaka Mtoto wa Miaka Miwili, Kumbaka Nguruwe, Mbwa na Farasi, Akakimbia Polisi Wakati Kesi Ikiendeelea. Mwaka 2012 Akapeleka Vyeti Vyake Kuomba Kazi Serikalini, Akakamatwa. Ilikuwa ni July 12, 2012 ambapo mji wa Somerton, Arizona US ulikuwa unatafuta vijana wa kuwasomesha na kuwaajiri kwa kazi ya doria, kulinda mipaka ya nchi hiyo, mmoja wa vijana waliopeleka maombi ya kazi hiyo alikua ni Cody Slaughter. Kijana huyo wa umri wa miaka 22 ilibidi akamatwe na polisi baada ya kupitia documents zake na kujua kuwa alikuwa ni mhalifu aliyetoroka Polisi ambapo hata alipokamatwa na kuhojiwa alikiri kuwa aliwahi kumdharirisha kingono mtoto wa umri wa miaka 2 miaka 8 iliyopita akiwa na miaka 14. Mbali na hilo pia Cody alikiri kuwa alikuwa na maingiliano ya ngono na mbwa, farasi na nguruwe, na alikuwa na historia ya utumiaji wa dawa za kulevya na baadaye mchinjaji. Licha ya kubainika na makosa hayo aliyoyafanya kati ya m...

Saddam Hussein|mtu akatwe mikono tu

Image
Akiwa Rais wa Iraq, Mwaka 1994 Saddam Hussein Alisign Adhabu ya Kupigwa Chapa Isiyofutika Usoni na Kukatwa Mikono, Miguu au Masikio Kama Utabainika Umeiba au Umehusika na Rushwa. Afisa Mmoja Alipigwa Chapa, Akaenda Kuifuta Hospitali, Madaktari Wote nao Wakakamatwa na Kukatwa Mikono. Mwaka 1997 Hussein Alitangaza Kuwa Ameandika Kitabu cha Qur'an kwa Kutumia Lita 27 za Damu Yake Aliyotumia Miaka 2 Kuitoa. Kuanzia Juni 4, 1994 serikali ya Iraq chini ya Saddam Hussein ilitoa amri tisa ambazo zikikiukwa tuu adhabu yake ilikuwa ni kali kama vile kukatwa viungo vya mwili, kupigwa chapa au adhabu ya kifo, baadhi ya  makosa yaliyopelekea adhabu hizo ni kama vile wizi, ufisadi au rushwa. Amri hizi mpya ziliathiri sana haki za binadamu lakini serikali ya Iraq ilipuuza ukosoaji mkubwa wa kimataifa wa ukatili huu kwa kusema kwamba amri hizo zilitungwa ili kupambana na uhalifu nchini humo ambapo unaleta vikwazo vya kiuchumi. Miaka hiyo ya 1990 afisa mmoja wa nchini humo alituhumiwa kwa rushwa na...

CLUB ILIYOIBA LOGO

Image
From fm facts Klabu ya Soka ya Olympic Burgas ya Burgaria Iliiba Logo ya Klabu ya Soka ya Ajax ya Uholanzi na Kuitumia Kama Logo Yao Pia, Tofauti Ilikuwa Majina tuu. Ajax Walivyolalamika Klabu Hiyo Ikaongeza Sigara Kwenye Mchoro wa Mtu Katika Logo Hiyo ili Kuweka Utofauti. Tazama Picha. Inaelezwa kuwa mchoro huo ni mchoro wa mungu wa Ugiriki ya kale, kwahiyo katika logo ya Olympic Burgas mungu huyo anavuta sigara.

KISA KELELE WAPANGIWA KUNYONGWA

Image
From Fm Facts Agha Mohammad Khan Qajar  Alikuwa Mfalme wa Iran (1789-1797). Mwaka 1797 Aliamuru Vijakazi Wake Wawili Wanyongwe Kisa tuu Walipiga Kelele Wakati Wakiongea. Kwakua Ilikuwa ni Mapumziko, Ikapangwa Wanyongwe Kesho Yake, Usiku Huo Huo Vijakazi Hao Wakamuuwa Mfalme Huyo. Note: Wakati huo Iran Ilikuwa Inaitwa Persia.

AUA MTU KISA MBU

Image
From Fm Facts April 27, 1982 Askari Woo Bum-kun wa Korea Kusini Alimuuwa Mpenzi Wake kwa Bahati Mbaya Baada ya Kumpiga Kifuani Akitaka Kumuuwa Mbu Aliyetua Hapo. Kwa Uchungu Jamaa Akaingia Mtaani Usiku Huo Huo na Kumuua Kila Mtu Aliyekutana Naye, Aliuwa Watu 56 na Kuwajeruhi Wengine 35, Naye Akajiuwa. Jina la mpenzi wake huyo ni Chun Mal-soon.

AULIWA MZIMA MZIMA😁

Image
from @fm_facts Jina lake halisi ni Hadj Mohammed Mesfewi maarufu kama Marrakesh Arch-Killer yaani muuwaji wa Marrakesh, Marrakesh ni moja ya miji mikubwa nchini Morocco. Haijulikani Mesfewi alizaliwa mwaka gani, lakini inakadiriwa tuu kuwa ni kati ya miaka ya 1850s hadi 1870s, alifariki kwa adhabu ya kifo June 13, 1906 baada ya kupatikana na hatia ya kuwauwa zaidi ya watu 36. Mesfewi alikuwa anafanya kazi kama fundi viatu na mfanyabiashara akisaidiwa na mwanamke wa miaka 70 aliyeitwa Rahali, alikuwa anawaalika wanawake kula nyumbani kwake, kisha anawapa dawa za kulevya na kuwaua wakiwa usingizini. Maiti 26 zilizokatwa na kijambia zilikutwa zimezikwa chini ya duka lake, wakati maiti zingine kumi ziliweza kugunduliwa chini ya majengo yake mengine ya biashara aliyokuwa nayo, haikujulikana sababu za kuuwa watu hao wote ni zipi. Inaelezwa kuwa Mesfewi alikuwa fundi viatu tuu, lakini nyuma yake alikuwa anamiliki maduka na biashara nyingi ambazo wengi hawakua wakizijua, na hata miili hiyo mi...