AULIWA MZIMA MZIMA😁

from @fm_facts

Jina lake halisi ni Hadj Mohammed Mesfewi maarufu kama Marrakesh Arch-Killer yaani muuwaji wa Marrakesh, Marrakesh ni moja ya miji mikubwa nchini Morocco.


Haijulikani Mesfewi alizaliwa mwaka gani, lakini inakadiriwa tuu kuwa ni kati ya miaka ya 1850s hadi 1870s, alifariki kwa adhabu ya kifo June 13, 1906 baada ya kupatikana na hatia ya kuwauwa zaidi ya watu 36.

Mesfewi alikuwa anafanya kazi kama fundi viatu na mfanyabiashara akisaidiwa na mwanamke wa miaka 70 aliyeitwa Rahali, alikuwa anawaalika wanawake kula nyumbani kwake, kisha anawapa dawa za kulevya na kuwaua wakiwa usingizini.

Maiti 26 zilizokatwa na kijambia zilikutwa zimezikwa chini ya duka lake, wakati maiti zingine kumi ziliweza kugunduliwa chini ya majengo yake mengine ya biashara aliyokuwa nayo, haikujulikana sababu za kuuwa watu hao wote ni zipi.

Inaelezwa kuwa Mesfewi alikuwa fundi viatu tuu, lakini nyuma yake alikuwa anamiliki maduka na biashara nyingi ambazo wengi hawakua wakizijua, na hata miili hiyo mingi alikua anaizika chini ya majengo yake ya biashara.

Ilimbidi Mesfewi auwawe Mei 2, 1906 baada ya kukamatwa, lakini kwakua watu walitaka auliwe kwa njia ya kikatili ili iwe fundisho ikabidi wasubiri hadi Juni 11, 1906 ambapo walimjengea kwenye ukuta kwa mawe na cement akiwa mzima huko Marrakesh.

Mesfewi alijengewa mwili mzima ukutani na kuachwa kichwa pekee ambapo baada ya kulia na kipiga kelele kwa siku mbili mfululizo akafia ukutani hapo, jamaa alifanywa tofali. Pichani ni vile inavyodhaniwa ilikuwa. Telegram link kwenye bio.

@fm_facts

Comments

Popular posts from this blog

KIFO NDIO KIWATENGENISHE

MFAHAMU MBAKAJI WA NGURUWE

TAJIRI MKUBWA DUNIANI