From @fmfacts

Kama kuna simulizi ya kukukumbukwa inayowatoa machozi raia wengi wa Colombia hasa wa miji ya Caldas na Tolima basi ni hii ya mtoto wa kike wa umri wa miaka 13 Omayra Sanchez iliyomtokea mwaka 1985. 


Omayra alikuwa ni mtoto aliyezaliwa August 28, 1972 huko Colombia na alifariki November 16, 1985 kwa mateso makali akiwa na umri wa miaka 13 huko Armero Columbia baada ya kukwama kwa siku 3 kwenye shimo lenye lava  kutokana na mlipuko wa Volcano uliotokea.

Janga hilo la volcano lililopewa jina la Nevado Del Ruiz lilitokea November 13, 1985 na kusababisha vifo vya zaidi ya Watu 25,000 Huku binti huyu wa miaka 13 pekee akikwama kwenye shimo ambapo volcano hiyo ilipita, unaweza kuvuta picha ya maumivu makali aliyoyapitia binti huyu.

Wakati mlipuko unaanza binti Omayra aliusikia, na alipokua anajitahidi kukimbia ili aepukane nao ndipo kwa bahati mbaya alijikuta ameingia ndani ya shimo lililopo karibu na nyumba yao, shimo ambalo lilikua na maji mengi pamoja na volcano dani yake, yaani ule uji uji wa moto, lava.

Hali hiyo ilimfanya akwame hapo huku akipitia maumivu makali, hata lilipokuja jeshi la uokowaji walijitahidi sana kadri ya uwezo lakini ilishindikana kutokana na hali duni ya vifaa hivyo vya uokowaji kwa wakati huo.

Zoezi la uokowaji la binti huyu lilidumu kwa muda wa siku tatu tangu Omayra akwame hapo  November 13, 1985, akafariki siku 3 baadaye akiwa hapo hapo baada ya kishindwa kusaidiwa.

Moja kati ya picha maarufu ya binti huyo akiwa shimoni hapo ilipigwa na mpiga picha wa kifaransa Frank Fourmer aliyekuwepo pia kwenye tukio hilo, Frank alisema:-


"Lilikua ni tukio la kusikitisha ambalo sikuwahi kushuhudia katika maisha yangu baada ya kuona hisia za mtoto yule akihangaika kujinasua huku akiwa analia, wakati  wakijitahidi kumuokoa alikua akifurahi akihisi ataokolewa na kuanza kuimba kwa furaha akihisi mda wowote ataokolewa katika janga hilo."

"Muda mwingine alionekana akisali akiwashukuru waokowaji kwani aliamini watamuokoa, lakini siku zilivyokuwa zinazidi kwenda bila mafanikio ndipo alipoanza kulia kwasababu alikua ameshakata tamaa ya kuokolewa, damu zilianza kumtoka na kuanza kubadilika macho yake rangi na kuwa meusi" Alisema Frank.

@fm_facts

Comments

Popular posts from this blog

KIFO NDIO KIWATENGENISHE

MFAHAMU MBAKAJI WA NGURUWE

TAJIRI MKUBWA DUNIANI